MozFest House: Kenya ni mkutano wa kikanda ambao utaleta pamoja wajenzi, watafiti, watunga sera, wanaharakati, mashirika ya kiraia, na uhisani ili waungane na kuchunguza masuala muhimu yanayohusiana na mtandao ulioboreshwa na AI inayoaminika. Jiunge nasi Nairobi, tarehe 21 hadi 22 Septemba 2023.
MozFest House: Kenya ni upanuzi wa kikanda wa MozFest, mkusanyiko wa kwanza wa wanaharakati, wasanii, wanateknolojia na waelimishaji katika harakati mbalimbali za kimataifa zinazopigania ulimwengu wa kidijitali unaozingatia masilahi ya kibinadamu. Likiendelezwa kutoka kwa MozFest House Amsterdam, hili litakuwa tukio la pili la MozFest House mwaka huu, lakini wakati huu, likilenga kanda ya Afrika Mashariki na Kusini.




Mazungumzo
Pata kufurahia mazungumzo ya kuchochea fikira na kuleta mazungumzo pamoja na viongozi wa jamii na maoni juu ya mwenendo wa mfumo ikolojia wa kidijitali na uvumbuzi unaoendelea katika Afrika ya Mashariki na Kusini. Hudhuria mjadala mkuu! Jishirikishe! Jadiliana na Hoji wataalamu!
Jinyakulie tiketi yako
Vikao vya ubunifu
Pata kuchochewa na ubunifu wa wazalishaji wa maudhui, wasanii, wajenzi, wabunifu na wajasiriamali wanaokubali kikamilifu teknolojia zinazohusika. Shirikiana na ujifunze kutokana na maonyesho mbalimbali na vikao vya mafunzo halisi kukiwemo na warsha na "hackathon" (tukio linalowaleta wasanidi programu za kompyuta pamoja).
Jinyakulie tiketi yako
Tukio la "The Barn"
Gundua mashirika mapya au shirikiana na wavumbuzi wapya, wanaharakati wa haki za kidijitali na washawishi na watunga sera katika mazingira tulivu kama ya shambani. Barizi palipo na hewa nyingi na nafasi ya kuanzisha ushirikiano huo!
Jinyakulie tiketi yakoRatiba
Ratiba itatolewa Agosti na itajumuisha warsha kadhaa za ushirikiano na za kuvutia, majadiliano na midahalo, mitambo ya sanaa, tukio la usanidi wa programu za tarakilishi, na mengi zaidi! Ikiwa wewe ni msanii, mtunga sera, mhadhiri, mwanaharakati, teknolojia au mtu anayetumia teknolojia nyumbani au kazi, kuna kitu cha kuchunguza.

Je, wewe ni mwenyeji wa eneo la Nairobi na una nia ya kujiunga nasi ili uweze kusaidia kuleta MozFest House: Kenya?
Jisajili ili ujitolee →

MozFest House: Kenya is taking place at Shamba Events
Shamba Events is a peaceful retreat from the bustling Nairobi traffic, with plenty of fresh air. The barn, stables and vast lawns are Ideal for events of any kind. It is located 100 meters beyond the entrance to Shamba Cafe & Shop along Loresho Ridge, just before the entrance to the University of Nairobi/VetLab Campus.